Jumanne 29 Septemba 2026 - 09:57
Mbunge wa Iraq atoa ombi la wazi kwa Serikali ya nchi hiyo

Hawza/ Suzan al-Saad, katika taarifa yake, ameeleza wasiwasi kuhusu madhara ya uamuzi wa kusitisha safari za ndege za Iran, na kusema: Tunaiomba Serikali ipitie upya maamuzi yake kuhusu kutokubali safari za ndege za Iran.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Suzan al-Saad, Mbunge wa Baraza la Wawakilishi la Iraq, katika taarifa yake ameonesha wasiwasi kuhusu madhara ya uamuzi wa kusitisha safari za ndege za Iran, na kusisitiza: Serikali inapaswa kuchunguza kiwango cha hasara za kiuchumi na kibinadamu zitakazotokana na uamuzi huu kwa nchi zote mbili.

Al-Saad amesema: Tunaelezea wasiwasi wetu kuhusu madhara ya uamuzi wa kusitisha safari za ndege za Iran, kuna uhusiano mwingi wa pamoja kati yetu na nchi jirani ya Iran, na hatua hii itavuruga uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Ameongeza kuwa: Iraq inapaswa kutekeleza jukumu chanya katika kutafuta njia za kupunguza mateso yanayotokana na mgogoro wa kiusalama, kiuchumi na kibinadamu, badala ya kuwaongezea wananchi wa Iran mizigo mipya. Kwa upande mwingine, vikwazo hivi vitaathiri pia uchumi wa Iraq, wakati ambapo nchi inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Najaf al-Ashraf, ambao hapo awali ulikuwa ukishuhudia kila siku safari za kawaida za takribani ndege 30 zilizokuwa zimewabeba mazuwari wa Iran, leo unakabiliwa na hatari ya kufungwa kabisa na kushindwa kabisa kugharamia gharama zake za uendeshaji kutokana na kusitishwa safari hizo.

Al-Saad ameendelea kusema: Hatua hii inahesabiwa kuwa ni kulengwa moja kwa moja maslahi ya kitaifa ya kiuchumi, hasara hii kubwa pia itasababisha kuvurugika kwa kiwango kikubwa muundo na maisha ya soko la ajira katika mikoa ya kidini, ambayo maisha ya maelfu ya familia humo yana uhusiano wa karibu na sekta ya utalii wa kidini. Kutokana na hilo, sekta za hoteli, migahawa na masoko ya kibiashara, pamoja na mtandao wa usafiri wa umma na binafsi, zitaathirika.

Ameeleza kuwa: Kwa sababu hiyo, tunaiomba Serikali ya Iraq ipitie upya maamuzi yake ya awali kuhusu kutokubali safari za ndege za Iran, ili isiweze kutafsiriwa kwamba leo tunasimama dhidi ya wananchi wa Iran waliowekewa mzingiro; wananchi ambao daima wamekuwa na misimamo chanya kwa wananchi wa Iraq.

Al-Saad ameendelea kusema: Aidha, tunaishawishi Serikali kuanzisha, kupitia njia za kidiplomasia, mazungumzo makubwa na ya moja kwa moja na upande wa Marekani, ili kupata misamaha itakayosaidia kulinda uchumi wa Iraq, kulinda taasisi za kitaifa dhidi ya hatari za vikwazo, na kupata suluhisho la msingi kwa uamuzi huu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha